Archive for February, 2009

last days in Berlin

February 24, 2009

last day in berlin party

last day in berlin party

Invitation to Maneno Mengi ‘An Evening of words and poems’

 

 

The Director of Goethe-Institut Tanzania invites you to the

 Poetry Evening event, which will be held on 12th March. 2009.

At the garden of the Goethe-Institut. Mrisho Mpoto ( Tanzania );

Sandra Mushi ( Tanzania ) – (poems recited by Maya Wegerif and

Langa Sarakikya);  Special Guest: Neema Mwatilo ( Kenya )

Followed by an Open Mic Session 

The concert will start from 07.00 p.m. evening.

 

 Yours sincerely

 

Ulrike Schwerdtfeger, Director

Goethe-Institut Tanzania

P.O. Box 9541, DSM

Tel. /Fax: +255 – 22 – 213 4800

Mobil: +255 – 782 502 190

info@daressalaam.goethe.org

 

 


Advertisements

Liyumba aibukia mahakamani

February 24, 2009

Hatimaye mtuhumiwa wa Wizi wa bilioni 221 kutoka kwenye ujenzi wa Magorofa ya benki Kuu ndugu yetu Liyumba ameibuka leo makakamani mweyewe bila zengwe baada ya kuingia mitini wiki iliyopita.

Liyumba sasa dhamana yake inajadiliwa na mahakama ya kisutu lakini dalili zinaonyesha hawatampa tena. Taarifa kamili badae kidogo kesi yake inaendelea mahakamani hivi sasa.

Last days in Berlin were emotional

February 23, 2009
Last diner hosted by IIJ

Last diner hosted by IIJ

Last days in Berlin were emotional!

February 23, 2009
This is class of 2007

This is class of 2007

At concentration camp where Hitler used to torture political prisoners
At concentration camp where Hitler used to torture political prisoners

Dk Slaa amwaga mawe tena ya ufisadi

February 22, 2009

Operation Sangara ya Chadema imeingia Dar es Salaam kwa Dk Wilbroad Slaa kumtaka Rais Kikwete amrudishe Liyumba alikomfisha.

Dk Slaa alikuwa akihutubia sokoni Kariakoo katika mkutano uliohudhuriwa na vijana kibao huku kiongozi mwingine wa chama hicho akijihutubia akihutubia upepo pale mnazi mmoja.

Kwa mujibu wa Slaa Liyumba katoroshwa na kufichwa na Serikali kama ilivyofanya kwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Daudi Balali ambaye potea kiaina.

Katibu huyo wa chadema pia ametaka Mzee wa vijisenti, Chenge ashughulikiwe hatua kwa kuchukua cha juu kwa kila mkataba aliosaini akiwa kama mwanasheria mkuu wa Serikali.

Eti chenge alikula cha juu kwenye ununuzi wa Rada na ndege ya Rais na mikataba mingine kibao aliyosaini kwa niaba ya Serikali na kuzificha New Jeyse Uk. Slaa anasema documenti zote za kuthibitisha anazo.

Halafu anasema eti wale Serious Fraud Office ya Uingereza walishamaliza uchunguzi kuhusu ufisadi wa chenge na walimkabidhi mwanasheria wa Tanzania Mwanyika lakini mpaka sasa hajachukuliwa hatua.

Hakuishia hapo alikwenda mpaka kumchokonoa Rais Mstaafu Mkapa kwamba anastahili kushitakiwa kwa 1: kufanya biashara akiwa Ikulu 2: kuchukua Kiwira kwa bei chee 3: kulazimisha wabunge waivunje NBC nay eye kuchota Milioni 500 kutoka ABSA kama cha juu.

Alisema mengi mpaka vijana walibaki mdomo wazi. Anataka wabunge wapunguziwe posho maana anaona ni dhambi kwa yeye kupokea 180,000 kwa siku wakati walimu wanapokea kiasi hicho kwa mwezi.

Operesheni samaki Sangara itaendelea tena mikoa ya kaskazini baada ya wiki mbili.

End

Kumbe alizama kwa brazameni!

February 22, 2009
Machozi band ya JD ikiwa kazini

Machozi band ya JD ikiwa kazini

Mshika mbunduki Thiery Henry akitafakari enzi hizo alikuwa na mwaka mmoja tu.Sikuhizi anapiga boli kwa kwenda mbele.
Mshika mbunduki Thiery Henry akitafakari enzi hizo alikuwa na mwaka mmoja tu.Sikuhizi anapiga boli kwa kwenda mbele.
Mshikaj Harid enzi hizo akiwa London ilibidi lazima akahiji Emirates
Mshikaj Harid enzi hizo akiwa London ilibidi lazima akahiji Emirates

Mambo ya Frankfurt burse!

February 20, 2009

wabongo na wafilipino wakiwa soko la Hisa, Frankfurt Germany

wabongo na wafilipino wakiwa soko la Hisa, Frankfurt Germany

This is inside Germany concentration camp where the Dictator Hitler used to torture political prisoners. Neutral Zone board shows the area where no prisoner was suppose to cross. Those who came closer to the neutral zone trying to reach the wall were short dead.
This is inside Germany concentration camp where the Dictator Hitler used to torture political prisoners. Neutral Zone board shows the area where no prisoner was suppose to cross. Those who came closer to the neutral zone trying to reach the wall were short dead.
Freddie Mercury mzaliwa wa Zanzibar akijulikana kama Farrokh Bulsara alikuja kuwa mwanamuzika mkubwa wa rocky duniani mwanzilishi wa kundi la the Queen Uingereza.Moja ya nyimbo alizoimba ni 'we will we will rock you'.Ukifika Unguja kuna club inaitwa Mercury na kuna picha zake ukutani kwa ajili ya kumbukumbu yake ukipata muda soma historia yake inatisha.
Freddie Mercury mzaliwa wa Zanzibar akijulikana kama Farrokh Bulsara alikuja kuwa mwanamuzika mkubwa wa rocky duniani mwanzilishi wa kundi la the Queen Uingereza.Moja ya nyimbo alizoimba ni ‘we will we will rock you’.Ukifika Unguja kuna club inaitwa Mercury na kuna picha zake ukutani kwa ajili ya kumbukumbu yake ukipata muda soma historia yake inatisha.

Mzee Liyumba aingia mitini baada ya dhamana

February 19, 2009

DHAMANA aliyopewa Amatus Liyumba imeingia dosari baada ya mahakama kutoa amri ya kukamatwa pamoja na wadhamini wake, lakini juzi na jana alisakwa na maafisa wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) lakini hakuonekana.

Alitakiwa apandishwe mahakamani jana, lakini badala yake maafisa wa takukuru waliambulia kuwakamata wadhamini na wakakiri mahakamani hapo kuwa Liyumba haonekani.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi ilitoa hati ya kukamatwa kwa Liyumba ikiwa ni siku moja tu baada ya kupewa dhamana na mahakama hiyo katika mazingira ambayo hayakuwaridhisha  upande wa mashitaka.

Hakimu Hadija Msongo jana alikiri kuwa mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamtwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake. Hata hivyo hakueleza sababu ya mahakama kutoa hati hiyo kwa kile alichodai kuwa jalada la kesi hiyo tayari limepelekwa mahakama kuu.

Jumanne Liyumba alipewa dhamana baada ya kuwasilisha mahakamani hapo hati ya mali yenye thamani ya Sh milioni 882 wakati alitakiwa kuwasilisha fedha taslimu Sh bilioni 55 au hati za mali zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Liyumba aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kusafiria ambayo muda wake wa kutumika umekwisha. Pia wadhamini wake wawili ambao walijitambulisha kuwa wanafanya kazi Benki Kuu hawakuwa na barua kutoka kwa mwajiri wao zaidi ya vitambulisho vyao vya kazi.

Licha ya Liyumba kutokamatwa na Takukuru, maafisa wa taasisi hiyo walifanikiwa kuwakamata wadhamini wake wawili ambao jana waliwekwa katika mahabusu ya mahakama hiyo kuanzia asubuhi hadi saa 10 alasri.

Wadhamini hao ni Otto Agatuangelus ambaye ni ofisa usalama wa ndani wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) pamoja na Mhasibu wa benki hiyo Benjamini Nguluguni.

Baadaye wadhamini hao walifikishwa mahakamani na hakimu Msongo anayesikiliza kesi hiyo akasema mahakama hiyo ilitoa amri ya kukamatwa kwa mshitakiwa na wadhamini wake ila kwa bahati mbaya jalada la kesi hiyo limepelekwa mahakama kuu.

Kwa hali hiyo, hakimu huyo alilazimika kuahirisha kesi hiyo hadi leo hii kusubiri jalada hilo litoke mahakama kuu na kurudishwa katika mahakama hiyo tayari kuendelea kwa shauri hilo. Aliwaamuru  wadhamini hao kwenda Mahakamani hapo tena leo kuelezwa kinachoendelea.  

Hakimu Msongo hakusema sababu ya kutoa amri ya kukamatwa kwa Liyumba kwani wakati akitoa dhamana kwa mshitakiwa huyo alipanga tarehe ya kurudi mahakamani kuwa ni Februari 24. Hata upande wa mashitaka haukueleza sababu ya kutolewa kwa hati hiyo ya kukamatwa mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake.

Hata hivyo wakati mahakama ilipotoa dhamana kwa mshitakiwa huyo, waendesha mashitaka wa serikali walidai kutoridhika na hatua hiyo kutokana na kuwepo mapungufu kadhaa katika hati alizowasilisha pamoja na hati yake yakusafiria.

Hata hivyo juzi mawakili wa Liyumba walizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa maamuzi ya mahakama ya kutoa dhamana kwa mteja wao yalikuwa ni halali kwa vile mteja alitimiza masharti ndio maana akaachiwa.

Masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama hiyo ni mshitakiwa huyo kujidhamini kwa fedha taslimu au hati ya mali hisiyohamishika yenye thamani ya Sh Bilioni 55. Sharti lingine ni kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria, haruhusiwi kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na awe na wadhamini wawili wanaofanya kazi katika taasisi inayotambulika.  

Wakati akiwa katika harakati za kudhaminiwa mawakili wake ambao wanaongozwa na Mgongo Fimbo waliwasilisha hati 11 za mali tofauti tofauti pamoja na kuwapeleka mahakamani wamiliki nane wa hati hizo.

Baada ya kuwasilishwa kwa hati hizo za dhamana upande wa mashtaka ulipinga kupokelewa kwa hati hizo kwa madai kuwa hazikuwa zimepitiwa na kufanyiwa uhakiki. Pia walidai hati hizo zina makosa yanayotakiwa kurekebishwa na ndipo walipoikubali hati moja ya nyumba iliyoko Mbezi jijini Dar es salaam ambayo inamilikiwa na mshtakiwa na yenye thamani ya Sh Miilioni 882.

Mawakaili wa Liyumba pia waliwasilisha hati ya kusafiria ya mshtakiwa huyo yenye namba A0320091 ambayo muda wake wa kutumika ulimalizika tangu Februari 12, 2007.

Baada ya mahakama kutoa dhamana hiyo waendesha mashitaka ambao hawakuridhika na uamuzi huo waliahidi kufanya kikao ili kujadili mwenendo wa suala hilo. Liyumba katika kesi hiyo anashitakiwa na Deogratius Kweka ambaye alikuwa mkurugenzi wa miradi wa BoT.

mwisho

Imeandikwa na Neema Mgonja.

 

Barafu ya kufa mtu Berlin!!

February 19, 2009

Faraja,
Kaka natumaini ni mzima na unaendelea kuwapa watu habari moto moto za kila siku, hii ndio hali halisi ya kila siku wakati huu wa baridi kila unapotembea ni Barafu tupu na utelezi wa kutisha, usipokuwa makini unaweza kuvunja kiuno bila kutarajia.  WAKATI HUU WATU WENGI SANA WANAUMIA KWA AJILI YA KUANGUKA  UTELEZI UMEZIDI SANA SNOW IKIGANDA INAKUWA KAMA KIOO NA INATELEZA SANA

WATU KIBAO PIA WANAKUFA KUTOKANA NA BARIDI KALI NA DALILI ZINAONYESHA MWAKA HUU NA WENGI WANATEGEMEWA KUFA KWA BARIDI. France, Berlin, Ugerumani

gari-3gari-ice-2gari-ice

wazee wa ulaya wanakaa nyumba maalum

February 18, 2009
wenzetu wazee wana nyumba zao serikali inawatunza.sisi je tutafika huko? hapa ni The Hague, Holland

wenzetu wazee wana nyumba zao serikali inawatunza.sisi je tutafika huko? hapa ni The Hague, Holland