MZEE WA Ze UTAMU AKAMATWA?

 POLISI wa Tanzania kwa kushirikiana na wenzao wa Kimataifa (Interpol) inadaiwa wamefanikiwa kumtia nguvuni kijana Malecela Peter Lusinde (39) kwa tuhuma za kuhusika na kuendesha mtandao uliojulikana kama Ze utamu ambao ulikuwa ukichapisha picha na habari zinazodhalilisha watu.

Mtandao huo ulifungwa na Serikali Februari mwaka huu baada ya malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu mtandao huo lakini mhusika alikuwa bado akitafutwa kutokana na kufanya makosa hayo.

Taarifa ambazo HabariLeo ilizipata jana zilisema kuwa Lusinde ambaye ni mtoto wa Waziri wa zamani wa Tanzania, alikamatwa hivi karibuni nchini Uingereza na amerudishwa nchini kujibu mashitaka hayo.

Lusinde ambaye anajulikana pia kwa jina la Male, ana uraia wa Uingerenza, ni mtaalamu wa Kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika kiingereza, Kiswahili na Kichina. 

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikina na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Lusinde na kupata ushahidi wa kutosha ndiye alikuwa mmiliki wa mtandao huo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa kumekuwa na malalamiko 7,000 kutoka kwa Watanzania wakisema kuwa mtandao huo ulikuwa ukidhalilisha watu na wakati mwingine mpaka viongozi wa juu Serikalini.

Halikadhalika mbali ya Lusinde, Polisi wa upelelezi walizungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego nchini Marekani, ambao pia wanahusishwa na mtandao huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Idara ya Upelelezi na Polisi wa Uingereza wamewaarifu Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza Clement Kiondo na Amos Msanjila.

Baadhi ya picha ambazo zilikuwa zikionyeshwa kwenye mtandao huo ni pamoja na za wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya juu nchini wakiwa UCHI.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s


%d bloggers like this: