Archive for the ‘General’ Category

MZEE WA Ze UTAMU AKAMATWA?

June 19, 2009

 POLISI wa Tanzania kwa kushirikiana na wenzao wa Kimataifa (Interpol) inadaiwa wamefanikiwa kumtia nguvuni kijana Malecela Peter Lusinde (39) kwa tuhuma za kuhusika na kuendesha mtandao uliojulikana kama Ze utamu ambao ulikuwa ukichapisha picha na habari zinazodhalilisha watu.

Mtandao huo ulifungwa na Serikali Februari mwaka huu baada ya malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu mtandao huo lakini mhusika alikuwa bado akitafutwa kutokana na kufanya makosa hayo.

Taarifa ambazo HabariLeo ilizipata jana zilisema kuwa Lusinde ambaye ni mtoto wa Waziri wa zamani wa Tanzania, alikamatwa hivi karibuni nchini Uingereza na amerudishwa nchini kujibu mashitaka hayo.

Lusinde ambaye anajulikana pia kwa jina la Male, ana uraia wa Uingerenza, ni mtaalamu wa Kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika kiingereza, Kiswahili na Kichina. 

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikina na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Lusinde na kupata ushahidi wa kutosha ndiye alikuwa mmiliki wa mtandao huo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa kumekuwa na malalamiko 7,000 kutoka kwa Watanzania wakisema kuwa mtandao huo ulikuwa ukidhalilisha watu na wakati mwingine mpaka viongozi wa juu Serikalini.

Halikadhalika mbali ya Lusinde, Polisi wa upelelezi walizungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego nchini Marekani, ambao pia wanahusishwa na mtandao huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Idara ya Upelelezi na Polisi wa Uingereza wamewaarifu Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza Clement Kiondo na Amos Msanjila.

Baadhi ya picha ambazo zilikuwa zikionyeshwa kwenye mtandao huo ni pamoja na za wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya juu nchini wakiwa UCHI.

Advertisements

Sitta aitaka Serikali kuleta uhuru wa habari

May 3, 2009

Sitta

Na Faraja Mgwabati

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Samuel Sita ametoa mwito kwa Serikali kuwasilisha Miswada ya Sheria zinazokinzana na dhana ya uhuru wa habari nchini ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa vyombo vya habari.

Akifungua Mkutano wa Siku ya Vyombo vya Habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Sitta alisema pamoja na hatua kubwa iliyopigwa, Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingi bado ina safari ndefu kufikia uhuru kamili wa vyombo vya habari.

Alisema kwa mfano, Sheria ya magazeti ya 1976 inampa Waziri mwenye dhamana ya habari kuvifungia vyombo vya habari huku sheria ya Usalama wa Taifa ya 1995 nayo inatoa mamlaka kwa Serikali kuingilia shughuli za vyombo hivyo pale vinapotoa habari zinazodhaniwa kuwa ni za kuhatarisha Usalama wa Taifa.

“Natoa wito kwa Serikali kuziwasilisha Bungeni Sheria zinazolalamikiwa ili ziweze kufanyiwa marekebisho na binafsi naahidi kuunga mkono jitihada zote zitakazoleta uhuru wa vyombo vya habari.

Hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba bila kuchelewa zaidi kwa Miswada ya Sheria za Haki ya Kupata habari na Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari inaletwa Bungeni na kujadiliwa,” alisema Sitta katika mkutano ambao uliandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN).

Spika alisema hatahivyo wanahabari lazima wakumbuke kuwa upatikanaji wa uhuru kamili vyombo vyao ni mchakato ambao wadau wake wakubwa ni wanahabari wenyewe kwakushirikiana na wanaharakati wa haki za binadamu na wananchi kwa ujumla.

“Hivyo hamna budi kwa njia ya majadiliano kuendelea kuishinikiza Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine ili ione umuhimu wa kuzifuta au kuzifanyia marekebisho ya sheria zinazolalamikiwa,” alisema Sitta.

Sitta aliwataka waandishi nao kufuata maadili ya taaluma ya Uandishi wa habari katika utekelezaji wa majukumu yao ama sivyo itakuwa ngumu kufikia ndoto ya kuwa na uhuru kamili wa vyombo vya habari.

“Nawasihi waandishi wa Habari tuzingatie miiko ya upashanaji habari. Tuepuke kuingiza chuki, uongo na ubinafsi katika taaluma na zaidi nawaomba wanahabari kukataa kutumika na wanasiasa na matajiri ili kutoa habari zisizo na tija kwa nchi yetu. Mtaheshimika pale tu na nyinyi mtajiheshimu na kuenzi taaruma yenu,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa MISA-TAN, Ayub Ryoba aliishauri Serikali kulitumia zaidi Baraza la Habari Tanzania (MCT) katika kutatua mambo mbalimbali badala ya kukimbilia kuvifungia vyombo vya habari.

End

Usafiri mwingine jamani unatisha

January 21, 2009
Taxi ikisanya kuelekea kijijini ikitokea Mbalizi Mbeya Kina mama wakiwa juu

Taxi ikisanya kuelekea kijijini ikitokea Mbalizi Mbeya Kina mama wakiwa juu

Mshika bunduki mtaalaam wa computer

January 21, 2009
Mshika Bunduki Thiery Henry Mgwabati anapenda kucheza na computer ingawa hata hajafikisha miaka miwili.

Mshika Bunduki Thiery Henry Mgwabati anapenda kucheza na computer ingawa hata hajafikisha miaka miwili.

Mila za wasafwa wa mbeya hizo

January 18, 2009
Mama wa Jamaa Charles Wilson (chungulia Chini) akiwa na wanae ambao nao hawajanyoa nywele kwa mwaka mmoja na nusu kwa ajili ya kutekeleza mila ya Wasafwa wa Mbeya ya kukaa miaka miwili bila kunyoa nywele ukizaa mapacha.

Mama wa Jamaa Charles Wilson (chungulia Chini) akiwa na wanae ambao nao hawajanyoa nywele kwa mwaka mmoja na nusu kwa ajili ya kutekeleza mila ya Wasafwa wa Mbeya ya kukaa miaka miwili bila kunyoa nywele ukizaa mapacha.

January 18, 2009
Mbeya vijijini kijiji cha Idimi kijana alikutwa akijivinjari ndani ya jezi maarufu 11 bila wasiwasi.Huwezi kujua anaweza kuja kuwa Gunners wa badae

Mbeya vijijini kijiji cha Idimi kijana alikutwa akijivinjari ndani ya jezi maarufu 11 bila wasiwasi.Huwezi kujua anaweza kuja kuwa Gunners wa badae

Mambo ya fish market

January 12, 2009
Hapa ni viunga vya Abuja mida ya jioni tukijivinjari na Kambare.Wenzetu kuna sehemu kama Mnazi mmoja pale kuna watu wanachoma kambare watamu kinoma wanapaita Fish market

Hapa ni viunga vya Abuja mida ya jioni tukijivinjari na Kambare.Wenzetu kuna sehemu kama Mnazi mmoja pale kuna watu wanachoma kambare watamu kinoma wanapaita Fish market

Mambo ya Abuja

January 12, 2009
Kitu kama hiki kingeletwa bongo, kitimoto isingeona ndani. Kambare anaokwa kitaalamu halafu anapasuliwa na kuchanganywa na chipsi plus pilipili! asikuambie mtu noma. Wenzetu Nigeria wanayohiyo.

Kitu kama hiki kingeletwa bongo, kitimoto isingeona ndani. Kambare anaokwa kitaalamu halafu anapasuliwa na kuchanganywa na chipsi plus pilipili! asikuambie mtu noma. Wenzetu Nigeria wanayohiyo.

Nani kasema Ulaya hakuna Ombaomba!

January 12, 2009
Mshikaji Ombaomba nilimkuta mlango wa kuingilia treni za chini ya ardhi nikamwomba nimpige picha alifurahi na kupozi.Hapa ni mtaa wa Oslerstrasher, Berlin Germany

Mshikaji Ombaomba nilimkuta mlango wa kuingilia treni za chini ya ardhi nikamwomba nimpige picha alifurahi na kupozi.Hapa ni mtaa wa Oslerstrasher, Berlin Germany

January 12, 2009
Ukifika Berlin be sure kumtafuta mshikaji France yupo peace kinoma atakupa michongo ya town. Hapa nipo naye kwenye train ananionyesha mji kidogo.Nimezoea kumwita mzee wa Spandau, moja ya mitaa ya Berlin, Germany

Ukifika Berlin be sure kumtafuta mshikaji France (Kulia) yupo peace kinoma atakupa michongo ya town. Hapa nipo naye kwenye train ananionyesha mji kidogo.Nimezoea kumwita mzee wa Spandau, moja ya mitaa ya Berlin, Germany